Baada ya kiongozi wa madansa kutoka WCB, Mosse Iyobo kumwita nyani Harmorapa, mwanamuziki huyo chipukizi ameamua kupiga picha akiwa na mdori wa nyani.
Harmorapa ameamua kupiga picha na mdori huo ili kumuonesha Mosse Iyobo kuwa kauli yake ilikuwa ya kidhalilishaji na ya kibaguzi kwa kuwa huwezi kumwita binadamu mwenzako nyani.
Wiki chache zilizopita Mosse Iyopo kupitia Instagram alicoment picha kwenye akaunti ya mtangazaji wa Clouds FM, B 12 na kumwita Harmorapa nyani kitendo ambacho kimemuzi msanii huyo chipukizi.
Mbali na hilo mwanamuziki huyo ameachia wimbo mpya aliomshirikisha Juma Nature unaitwa ‘Kiboko ya Mabishoo’ ambapo baadhi ya mistari ya nyimbo hiyo amemdisi Mosse Iyobo pamoja na Aunty Ezekiel pamoja na kundi zima la WCB.
Wimbo huyo umefanywa kwenye studio za Mr T. Touch ambao umetoka leo na kuanza kuchezwa kwenye vituo mbali mbali vya radio hapa nchini.