Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), imezitaka mamlaka za miji kuweka sawa miundombinu ya kupitisha maji kufuatia mvua zinazonyesha ili kuondoa uwezekano wa kutokea mafuriko ambayo yanaweza kuathiri jamii.

TMA imezishauri Mamlaka ya Maafa na wadau wengine kuchukuwa hatua stahiki katika utunzaji wa mazingira, mipango na kujiandaa kukabiliana na majanga yanayoweza kutokea kutokana na mwenendo wa mvua.

Mkurugenzi Mkuu wa TMA, Dk. Agnes Kijazi, alisema mamlaka hizo na wananchi wanashauriwa kuhakikisha wanajiandaa kwa kuweka sawa mindombinu inayowazunguka ili kujihakikishia usalama wakati wa mvua za masika ambazo zinatarajiwa kuwa kubwa katika baadhi ya mikoa.

Aidha mkurugenzi huyo aliongeza kuwa kutoakana na hali ya ukame ulioyakumba maeneo mengi ya nchi, sasa yanaweza kupata mvua, hivyo wanatakiwa kupata ushauri wa maofisa kilimo kujiandaa kwa kilimo.

Ukanda wa Pwani ya Kaskazini unatarajiwa kuwa na mvua za wastani hadi chini ya wastani, vipindi virefu vya ukavu na mtawanyiko hafifu wa mvua katika baadhi ya maeneo hayo,” alisema.

Kwa mujibu wa Dk. Kijazi, mikoa ya Kanda ya Ziwa Viktoria inatarajiwa kuwa na mvua za wastani hadi juu ya wastani, huku Nyanda za Juu Kusini zikitazamiwa kuwa na mvua za wastani au chini ya hapo.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *