Rais wa shirikisho la soka duniani Fifa, Giani Infantino amesema kuwa Afrika itapewa nafasi za timu 7 zitakazoshiriki katika kombe la dunia mwaka 2026.

Infantino amesema kuwa shirikisho hilo limeongeza uwekezaji wake Afrika kutoka dola milioni 27 hadi 94 kwa mwaka ili kusaidia kukuza mchezo huo.

Giani Infantino yuko nchini Ghana kwa ziara ya siku moja ambapo awali alifungua ujenzi hoteli ya chama cha soka nchini Rwanda.

Amekuwa akikutana na rais Akufo Addo na maafisa wakuu wa shirikisho la soka nchini Ghana kuzungumzia hatua za kukuza soka nchini humo.

Ziara yake ni mojawapo ya ziara za mataifa kadhaa wanachama wa Fifa ambapo amesema kuwa uongozi wake umedhamilia kukuza soka la Afrika na dunia kwa ujumla.

Hapo awali Afrika ilikuwa inaingiza timu tano kwenye michuano ya kombe la dunia lakini kwasasa itaingiza timu mbili kwenye michuano hiyo mikubwa duniani.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *