Taasisi inayotoa tuzo za Utawala bora ya MO Ibrahim imetangaza kukosa mshindi kwa mwaka 2016, inayotolewa kwa viongozi wa Afrika waliostaafu.

Hayo yamesemwa kwenye mkutano  wa kamati  uhuru  ya tuzo hiyo, chini ya mweyekiti wa Dr Salim Ahmed Salim pamoja na  mkutano wa  bodi ya  taasisisi hiyo iliofanyika  mwishoni mwa wiki lililopita.

Akizungumzia juu ya uamuzi wa kamati  ya tuzo hiyo ya Mo Ibrahim, Dr Salim alisema ” kama  ninavyosisitiza kila mwaka , paliwekwa kipimo cha hali ya juu, wakati tukizindua tuzo hii  2006.

Dr Salim akaongeza kusema kwamba baada ya zingatio makini, kamati hiyo imeamua  kutomzawadia yeyote tuzo hiyo kwa  mwaka 2016.

Wagombea wote wa  tuzo ya Ibrahim ni ama Viongozi  wa taifa  au Serikali waliondoka madarakani katika kipindi cha miaka mitatu iliopita  na ambao walikuwa wamechaguliwa kidemokrasi na kutumikia vipindi vyao kwa mujibu wa katiba.

Tangu ilipoanzishwa 2006, tuzo ya Mo Ibrahim imeshatolewa mara nne. Washindi waliopita  ambao wote walikuwa marais wa nchi zao ni, Hifikepunye Pohamba wa Namibia (2014), Pedro Pires wa visiwa vya Cape Verde (2011), Festus Mogae wa Botswana  (2008) na Joaquim Chissano wa Msumbiji (2008). Rais wa zamani wa Afrika Kusini Hayati Nelson Mandela alitunukiwa  tuzo ya heshima  2007.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *