Wizara ya Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira imesema kuanzia kesho atakayekutwa na pombe aina ya viroba atachukuliwa hatua.

Tamko hilo lililotolewa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alivyoagiza kuondoa vifungashio vyote vya pombe kali aina ya viroba.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Muungano January Makamba kwa kusema ametoa onyo kuwa atakayeendelea kuvisambaza mitaani atachukuliwa hatua kali kuanzia kesho.                        

Makamba amesema kuwa oparesheni juu ya katazo hilo utazingatia ibara ya 8(1) b na 14  sheria ya mazingira ya mwaka 2014 na kanuni zake.

Makamba ameeleza kuwa Oparesheni ya Kukagua Utekelezaji wa Agizo la Serikali la Usitishaji, Utengenezaji, Uuzaji na Matumizi ya Pombe zinazofungashwa kwenye vifungashio vya plastiki itaendeahwa nchini kote kuanzia Machi 2, 2017 kupitia kamati za ulinzi na usalama na kamati za mazingira katika ngazi ya mikoa, wilaya, tarafa, kata na vijiji.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *