Rais wa Gambia, Adama Barrow amemfuta kazi mkuu wa majeshi Jenerali Ousman Badjie ambaye alikuwa chini ya uongozi wa rais Yahya Jahmmen.

Jenerali Badjie ametangaza utiifu wake kwa rais aliyeondoka madarakani Yahya Jammeh baada ya uchaguzi wa Disemba ulioleta vuta nikuvute.

Hata hivyo, chini ya amri yake, jeshi halikutoa msaada wowote pindi vikosi kutoka nchi za Afrika Magharibi vilipoingia nchini Gambia mwezi jana.

Vikosi hivyo vilifanikiwa katika kumshawishi bwana Jammeh kukubali kushindwa na kuondoka nchini.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *