Rais wa Uganda, Yoweri Museveni amemhakikishia Rais Magufuli kuwa yupo tayari kuweka jiwe la msingi la mradi wa ujenzi wa bomba la mafuta kutoka Hoima nchini Uganda hadi Bandari ya Tanga nchini Tanzania.

                                                                                                                                                           Rais Museveni amesema hayo jana katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam wakati akiagana na mwenyeji wake Rais Magufuli baada ya kumaliza ziara yake rasmi ya kiserikali ya siku 2 hapa nchini na kurejea Uganda.

Rais Museveni aliwasili nchini juzi asubuhi ambapo amefanya mazungumzo na mwenyeji wake Rais Magufuli na jana ametembelea viwanda viwili vinavyomilikiwa na kampuni ya mfanyabiashara wa Tanzania Bw. Said Salim Bakhresa ambavyo ni kiwanda cha uzalishaji wa unga wa ngano kilichopo Buguruni na kiwanda cha uzalishaji wa juisi kilichopo Vingunguti Jijini Dar es Salaam.

 

Licha ya kuwekeza nchini Uganda Mfanyabiashara huyo pia amekuwa akipeleka bidhaa zake kwa wingi nchini Uganda.

 

Pamoja na Mhe. Rais Magufuli viongozi wengine waliokuwepo wakati wa kumuaga Mhe. Rais Museveni ni pamoja Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Majaliwa na Viongozi wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *