Rais wa Marekani Donald Trump amesema hatahudhuria dhifa ya chakula cha jioni inayoandaliwa na chama cha waandishi wa habari wanaoripoti matukio ya Ikulu.

Tangazo la Trump linakuja siku moja baada ya kuwashutumu vikali wanahabari kwa kuwataja kuwa ni adui wa watu kwa kudai wanaeneza taarifa za uongo na za kupotosha.

Kiongozi huyo mpya wa Marekani pia amewataja wanahabari kuwa chama cha upinzani nchini Marekani.

Dhifa hiyo iliyoanzishwa mwaka 1921, huwa inahudhuriwa na watu mashuhuri, wanasiasa wa Marekani na wanahabari.

Rais wa chama cha waandishi wa habari wa Ikulu ya White House WHCA Jeff Mason amesema dhifa hiyo itaendelea kama ilivyopangwa kwani ni desturi ya kusherehekea mchango muhimu unaotekelezwa na mashirika ya habari katika taifa lililo huru..

Msemaji wa Ikulu Sean Spicer mnamo siku ya Ijumaa aliwazuia wanahabari wa mashirika kadhaa kuhudhuria kikao cha wanahabari katika Ikulu.

Wanahabari wa Mashirikia ya CNN, New York Times, Politico, Los Angeles Times na Buzzfeed hawakuruhusiwa kuhudhuria kikao cha wanahabari katika ofisi ya msemaji wa Ikulu ya Rais wa Marekani.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *