Muigizaji nyota wa Bongo Movie, Jacqueline Wolper amesema kuwa marafiki wapya katika maisha ndio chanzo cha wanaoharibu misingi ya maisha yake.

Wolper amesema kwamba, wakati wa kupata marafiki wapya huwa mzuri lakini baadaye hujikuta katika matatizo yasiyokwisha.

Pia amesema “Sisi mastaa tuna kazi kubwa, kila siku tunakutana na marafiki wapya ambao kati yao wapo wahalifu wanaojificha kupitia majina yetu na linapotokea jambo baya hujikuta ukijumuishwa ukiwa hujui chochote.

Wolper amesema kuwa “Nawashauri mastaa wenzangu wa fani zote kuwa makini na marafiki kwa kuwa wengi wao hututumia kwa maslahi yao na katika mambo mengi tusiyoyajua,”.

Muigizaji huyo amesema hayo baada ya kupata kashfa nyingi kutokana na tabia yake ya kubadilisha marafiki ambao wamekuwa chanzo cha kumualibia maisha yake kwa sababu wengine ni marafiki wanafki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *