Kocha wa Manchester United, Jose Mourinho amewashutumu wachezaji wa Leicester kuwa na ubinafsi wa kumsaliti aliyekuwa kocha wao Claudio Ranieri.

Mourinho alivaa kofia yenye nembo za CR akimuunga mkono Claudio Ranieri kabla ya kuwashutumu wachezaji hao ambao wengi wao walisaini mkataba mpya baada ya kushindi taji la ligi.

Muorinho alifukuzwa Chelsea katika mandhari kama hayo msimu uliopita kufuatia mgomo wa wachezaji lakini akasema kuwa kisa alichofanyiwa kilikuwa kidogo sana ikilinganisha na vile Ranieri alivyofanyiwa.

”Nadhani msimu huu ulianza na ubinafsi mwingi wachezaji wakitaka kupewa mikataba mipya” Mourinho amesema.

”Watu wakifikiria fedha zaidi wengine wakiamua kuondoka bila kujali ni nani aliyewafanya kufikia walivyo” aliongeza Mourinho.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *