Rais wa Afrika Kusini, Jacob Zuma amesema kuwa amesikitishwa na tabia ya raia wa nchi hiyo kuwashambulia wageni walioko nchini Afrika kusini.

Zuma amesema kuwa raia wengi wa kigeni wanaoishi Afrika Kusini, ni watu wanaoheshimu sheria na kuchangia pakubwa katika ukuaji wa uchumi wa taifa hilo.

Amesema ni makosa kwa raia wa nchi hiyo kuwaona wageni kama ni walanguzi na watumiaji wa mihadarati.

Licha ya kauli hiyo ya rais Zuma waandamanaji tayari wamefunga barabara mjini Pretoria kwa kuchoma tairi za magari wakijiandaa kwa maandamano ya kupinga kile wanachotaja hali ya wenyeji kupoteza nafasi za kazi kwa wageni.

Wiki chache zilizopita ripoti zilizotoka ambazo zimesema zaidi ya raia 120 wa nigeria wameuawa kwa kipindi cha miaka mitatu toka kutokea kwa machafuko hayo nchini humo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *