Muigizaji wa Bongo Movie, Wastara Juma ametapeliwa milioni 84 na kampuni moja ya simu ya Wachina baada ya kuingia nao mkataba wa kuwa balozi wao hapa nchini.

Wastara aliingia mkataba na Wachina hao mwaka jana ambapo alitakiwa awe analipwa shilingi milioni 400 kwa mwaka lakini ghafla Wachina hao wakaingia mitini.

Muigizaji huyo amesema kuwa Pesa ambayo anawadai ni milioni 84 kwasababu kabla ya wachina hao kuja  nchini walitaka aanze kutumia pesa zake  kuandaa tisheti, kofia na mambo mengine ya kipromosheni.

Wastara ambaye ni mpenzi wa Bond amesema kuwa  ilipopita miezi mitatu bila kuona maendeleo yoyote alianza kuwasiliana nao tena, wakaanza kumletea Kiswahili kingi, nikashtuka na kuweka mwanasheria wangu amba ambaye alikuwa nao sambamba, napo wakajaribu kumnyamazisha kwa pesa wakashindwa.

Akaongeza kuwa, mara ya mwisho walikwenda kwenye kikao cha kujua hatima ya malipo yake na kinachoendelea ndipo afisa masoko wa kampuni hiyo aliyefahamika kwa jina la Raymond Kalika alipomwambia kuwa Wachina hao wamerudi kwao.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *