Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam, (UDSM) kimesema kuwa hakuna mwanafunzi hata mmoja aliyedahiliwa chuoni hapo ambaye hana sifa za kujiunga na chuo hicho.

Naibu Makamu Mkuu wa Chuo hicho, Profesa Florens Luoga amesema kuwa UDSM kimeweka utaratibu ambao unaweza mwanafunzi yeyote anayedahiliwa chuoni hapo, awe na sifa zinazohitajika kwa kuwa hawafanyi biashara.

“Sisi hapa ni wakali kuhusu jambo hilo, tukibaini kuwepo kwa mwanafunzi ambaye hana sifa tunamfukuza. Hatusubiri TCU iseme…hata tukibaini kuwa mtu alifanya udanganyifu na alishamaliza chuo, lakini hakuwa na sifa, tunamnyang’anya digrii tulivyompa,” alisema Profesa Luoga na kuongeza:

Amefafanua kuwa kuna baadhi ya programu maalumu, ambazo Serikali ya Tanzania imeingia na nchi nyingine kwa ajili ya kuendesha programu maalum.

Pia amesema kozi hizo zimekuwepo chuoni hapo kwa muda wa miaka 40 sasa na zinafanywa kutokana na makubalino ya Serikali ya Tanzania na nchi husika.

Amesema chuo hicho kikongwe Tanzania, kutokana na kuwepo makubaliano hayo kimekuwa kinapokea baadhi ya wanafunzi ambao wanatoka nje ya nchi na akasisitiza kuwa yawezekana ndio hao ambao TCU imeshindwa kupata nyaraka zao.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *