Muigizaji nyota wa Bongo Movie, Irene Uwoya amesema kuwa ana mpango wa kuwa Mchungaji pamoja na kumiliki kanisa lake yeye mwenyewe siku za usoni.

Uwoya pia amefunguka na kueleza kuwa kazi yake ya sanaa huwa inamtesa kiimani jambo ambalo linamfanya kila siku akiamka awe anatubu kwa ajili ya mambo anayoyafanya akiwa katika kazi zake za uigizaji .

Amesema katika tasnia ya uigizaji mara nyingi huwa wanaongea uongo na hata mambo mengi wanayoyafanya kufikisha ujumbe huwa ni vitu ambavyo havimpendezi Mungu.

Kwa upande mwingine Uwoya amesema kuwa dawa za kulevya na hajawahi kutumia kwa kuwa ni mkristo na dini yake hairuhusu kutumia dawa za kulevya wala kushiriki katika ndoa za jinsia moja lakini pombe anakunywa.

Pia amefunguka kuhusu mapenzi yake ya kuvaa nguo fupi ambapo amesema anapeda nguo fupi, kwa kuwa ana mzio aleji na nguo ndefu hivyo hawezi kuvaa nguo ndefu.

Mbali na Uwoya Nay wa Mitego naye ni miongoni mwa wasanii wenye ndoto ya kufungua kanisa siku za usoni.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *