Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe amesema kuwa anahitaji nchi irejee katika misingi ya utawala wa katiba, sheria na utaratibu.

Freeman Mbowe kupitia mitandao ya kijamii amesema kutokana na jina lake kuhusishwa na tuhuma za dawa za kulevya bila ushahidi katika hilo ni lazima adai haki yake kwa kuchafuliwa jina lake.

Mbowe amezungumza hayo ikiwa ni siku moja baada ya mahakama kulizuia jeshi la polisi kumkamata hadi hapo kesi yake ya kikatiba itakapoamuliwa.

Mbali na hilo Freema Mbowe amesema kwa sasa anapambana na dola, anapambana na serikali vyombo vya usalama pamoja na mkuu wa mkoa lakini anatambua kuna watu wengi wanapata shida kama yeye lakini hawana uwezo wa kudai haki zao hivyo yeye mapambano yake ni ni katika kupigania haki katika taifa ili taifa liendeshwe kwa mujibu wa katiba, sheria na utaratibu wa nchi na si vinginevyo.

Mbowe amefungua kesi mahakama kuu dhidi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Kamishna Simon Sirro na Mkuu wa Upelelezi wa kanda hiyo, Camilius Wambura.

Mbowe ni miongoni mwa watu waliotajwa na mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda wanaojihusisha na baishara ya dawa za kulevya ambapo alikamatwa na jeshi la polisi kwa ajili uchunguzi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *