Rais wa Marekani, Donald Trump na viongozi wengine wa Uturuki, Hungary na Ufilipino wameshtumiwa na Shirika la Amnesty International kwa kuwatumia wakimbizi kwa manufaa yao ya kisiasa.

Kutokana na taarifa ya Shirika hilo viongozi hao wanaendeleza kile inachokitaja kuwa kuwatumia vibaya wakimbizi kwa manufaa yao ya kisiasa badala ya kutanzua kiini hasa kilichowafanya wakimbizi hao kuyakimbia mataifa yao.

Shirika hilo limeelezea mwaka 2016 kama mwaka wa matamshi yaliyojaa chuki huku hofu ikapanda zaidi na kufikia kiwango ambacho hakijawahi kufikia tangu miaka ya 1930, wakati Adolf Hitler alipoingia madarakani nchini Ujerumani.

Ripoti hiyo inapinga sera ambazo zinakubalia ubaguzi wa rangi na chuki unaofanywa na viongozi wa mataifa hayo ndani ya nchi zao.

Ripoti hiyo inasema mataifa mbalimbali duniani yanaendesha ajenda potovu ambayo inawahujumu wakimbizi ambao wanashutumiwa kwa makosa ambayo hawakutenda huku pia wakidhulumiwa kijumla.

Shirika hilo la kutetea haki za binadamu duniani limetoa ripoti hiyo kutokana na vitendo vya mataifa hayo kuwanyanyasa wakimbizi badala ya kutatua matatizo yao.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *