Manchester City imeanza vizuri hatua ya 16 bora baada ya kushinda 5-3 dhidi ya Monaco kwenye mechi ya klabu bingwa barani Ulaya iliyofanyika katika uwanja wa Etihad jana.
Manchester City ndiyo iliyokuwa ya kwanza kupata goli baada ya kiungo wake Raheem Stearling kupachika bao katika dakika ya 26 ya mchezo huo.
Magoli mengine ya Manchester City yamefungwa na Sargio Aguero aliyeshinda magoli mawili dakika 58 na 71, Stone dakika ya 77 huku goli la mwisho likifungwa na Sane katika dakika ya 88 ya mchezo huo hapo jana.
Mechi nyingine Bayern Leverkusen imefungwa 4-2 na Atletico Madrid katika mechi iliyofanyika katika uwanja wa BayArena.
Michuano hiyo ya Ulaya itaendelea tena leo kwa michezo mingine miwili kupigwa FC Sevilla watakuwa mwenyeji wa Leicester City huku FC Porto watawakaribisha Juventus.