Kesi inayomkabili Mkurugenzi na Mwanzilishi wa Kampuni ya Jamii Forum Media Limited, Maxence Melo (40) upelelezi wake umekamilika.
Kesi hiyo imeahirishwa hadi Machi 13 mwaka huu, baada ya upande wa mashitaka kuomba muda wa kujipanga zaidi ili kusoma maelezo ya awali ya mshitakiwa.
Wakili Mwandamizi wa Serikali, Mohammed Salum amedai katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, mbele ya Hakimu Mkazi, Godfrey Mwambapa kuwa kesi hiyo imekuja kwa ajili ya kutajwa na upelelezi wa shauri hilo umekamilika.
Pia aliomba tarehe nyingine kwa ajili ya kujipanga kumsomea mshitakiwa maelezo ya awali. Hakimu Mwambapa aliahirisha kesi hiyo hadi Machi 13 mwaka huu, kwa ajili ya kusomewa maelezo ya awali.
Melo anakabiliwa na mashitaka manne katika mahakama hiyo kwa mahakimu watatu tofauti ambao ni Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba, Hakimu Mkazi, Victoria Nongwa na Hakimu Mwambapa.
Pia inadaiwa mshitakiwa alizuia jeshi hilo kufanya uchunguzi kinyume na Sheria Namba 22 (2) cha Sheria ya Makosa ya Mtandao Namba 14 ya mwaka 2015.
Wakili Salum amedai kuwa, kati ya Desemba 9, 2011 na Desemba 13 mwaka jana, maeneo ya Mikocheni wilayani Kinondoni, akiwa Mkurugenzi wa kampuni hiyo, alisajili tovuti ya Jamii Forum kwa kikoa cha .com badala ya .co.tz jambo ambalo ni kinyume cha sheria.