Serikali imesema itaweka mikakati madhubuti ya kutangaza madini ya tanzanite nje ya nchi ili kujulikana zaiid.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ameyasema hayo mwishoni mwa wiki katika mkutano wa hadhara uliofanyika Uwanja wa Getini, Mirerani.

Aidha katika mkutano huo alisisitiza kuwa serikali pia itahakikisha madini ya Tanzanite yanayopatikana Tanzania yanatangazwa na kujulikana duniani kote na kuwanufaisha wajasiriamali wadogo na wazawa.

Amesema, madini ya tanzanite yanayopatikana pia India yanajulikana zaidi duniani kuliko yanayopatikana Mirerani, na kwamba Serikali itaangalia upya ya sheria inayoruhusu kampuni za nje yanayonunua madini hayo katika ulipaji kodi ili halmashauri husika zipate mapato ya ndani na serikali kupata mapato kutokana na minada ya madini hayo na uwekezaji.

Waziri Mkuu amesema, imegundulika kuwa sekta ya madini ina matatizo mengi na migongano kati ya wachimbaji wadogo na wakubwa na upatikanaji wa leseni za makundi hayo ambapo sheria ya madini nchini inasisitiza wachimbaji na wawekezaji kuwa na leseni jambo ambalo alisema litafanyiwa kazi ikiwa ni pamoja na kujua wawekezaji wameingiaje katika maeneo hayo, leseni zao zimepatikana wapi na mfumo wa ulipaji kodi wao.

Alisisitiza kuwa azma ya serikali ni kuona inawainua wajasiriamali wadogo wa machimbo ya madini ikiwamo kuwa na zana bora za uchimbaji kwa kutambulika kisheria, na ili wafanye kazi hizo za uzalishaji ni lazima waondokane na maambukizi ya ugonjwa wa Ukimwi ambayo kwa Mirerani pekee maambukizi hayo yako juu kwa asilimia 18.

Akiwasilisha taarifa ya Wilaya ya Simanjiro mbele ya waziri Mkuu, Mkuu wa wilaya hiyo, Zephania Chaula alisema wachimbaji wa tanzanite baadhi yao hawatoi takwimu sahihi za uzalishaji zinazoiwezesha halmashauri kukusanya kodi ya huduma kutokana na utoroshaji wa madini hayo nje ya wilaya na nje ya nchi.

 

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *