Waziri wa Katiba na Sheria, Dkt. Harrison Mwakyembe amesema kuwa mtu yeyote atakayekutwa na shamba la banngi  anaweza kuhukumiwa kifungo cha kuanzia miaka 30 gerezani.

Adhabu hiyo ni kwa mujibu wa Sheria Mpya ya Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na dawa za kulevya ambayo imeanza kutekelezwa hivi karibuni.

Mbali na adhabu hiyo, sheria hiyo pia imeweka adhabu ya kifungo cha maisha kwa mtu atakayebainika kusafirisha aina yoyote ya dawa za kulevya, pamoja na wale wanaoingiza dawa kutoka nje ya nchi.

Pia sheria hiyo inatoa adhabu ya faini ya shilingi milioni 200 na kifungo cha maisha kwa watakaokutwa na malighafi au maabara za kutengezea dawa za kulevya huku ikiweka adhabu ya kifungo cha miaka mitano na/au faini ya kuanzia shilingi milioni moja kwa mtu atakayekutwa na kiasi kidogo cha dawa cha dawa za kulevya.

Amesema lazima kutakuwa na ukosoaji kwa kuwa sheria hiyo ni mpya hasa katika suala la mashahidi, lakini kuna sheria nyingine ya kulinda mashahidi (Whistle Blowers Act), ambayo itasaidia kuwalinda watu wanaotoa taarifa kuhusu wahusika wa dawa za kulevya.

Amesema pia serikali iko tayari kupokea maoni kutoka kwa wadau, juu ya nini kifanyike ili kuwadhibiti wahusika wa dawa za kulevya ambao wamekuwa wakiifanyia wema jamii inayowazunguka kwa kiasi kikubwa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *