Watu 34 wameuawa na wengine 50 kujeruhiwa katika mlipuko wa bomu lililotegwa ndani ya gari mjini Mogadishu nchini Somalia.
Kwa mujibu wa idara za usalama nchini humo gari hilo lililokuwa na milipuzi lilifanya shambulio hilo katika mtaa wa Madina kusini mwa Somalia.
Shambulio hili ni la kwanza kufanyika katika utawala mpya wa taifa hilo wa Somalia chini ya Rais wa Mohamed Abdullahi Mohamed.
Hakuna kundi la kigaidi ambalo limekiri kuhusiana na tukio hilo, japo kuwa kundi la al Shabaab linatiliwa shaka kuhusika na shambulio hilo.
Siku ya jumamosi kamanda mwandamizi wa al shabab alitangaza kuwa watafanya shambulizi kulenga wafuasi wa rais.