Wanachama 300 wa mwisho wa kundi kuu la wapiganaji wa msituni nchini Colombia, FARC, wamewasili katika kambi ya kurekebisha tabia ili wajumuishwe tena na raia.

Mwaka jana kundi la wapiganaji wa FARC, lilitia saini muafaka wa amani na serikali ya nchi hiyo, ili kumaliza uhasama wa mwagaji damu, uliodumu miongo kadhaa.

Takriban wapiganaji elfu 7 wameingia katika vituo zaidi ya 20, vya urekebishaji tabia na kukubalika katika jamii, baada ya kutembea mwendo mrefu kutoka maeneo ya milima milima na msituni, walikokuwa.

Lakini Umoja wa mataifa, umeonyesha wasiwasi wake kuwa kambi hizo haziko tayari kuwapokea waasi hao.

Maafisa walikuwa wameomba serikali ya Colombia kuchelewesha kwa muda ratiba ya kusalimisha silaha, hadi pale silaha za kundi hilo la FARC, zimechukuliwa na kuhifadhiwa mahala salama kwanza.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *