Rais wa Marekani, Donald Trump amevishambulia vyombo vya habari katika mkutano wa kisiasa nchini Marekani katika jimbo la Florida nchini Marekani.

Aliuambia umati mjini Melbourne kwamba vyombo vya habari havitaki kabisa kusema ukweli na kwamba waandishi wa habari wana ajenda zao fiche.

Pia Trump ametetea mafanikio ya utawala wake, akisisitiza kuwa sasa yeye ni “kinara wa roho ya matumaini inayokwenda kwa kasi kote Marekani, huku akirejelea ahadi nyingi alizotoa wakati wa kampeni yake kuhusiana na ufufuaji wa uchumi na uimarishaji wa usalama.

Rais Donald Trump leo Jumapili atawahoji watu ambao watasimamia nyadhifa nne za washauri wa kitaifa wa maswala ya usalama.

Watu hao wanamjumuisha Keith Kellogg kaimu mshauri mkuu wa usalama wa kitaifa, baada ya kutimuliwa kwa Michael Flynn juma lililopita na Balozi wa zamani wa Marekani katika umoja wa mataifa John Bolton.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *