Serikali imesema ina mpango wa kukarabati uwanja wa ndege wa Mtwara ifikapo mwezi Julai mwaka huu ili kuruhusu ndege kubwa kuweza kutua uwanjani hapo na hivyo kufungua fursa za kiuchumi mkoani humo.
Akizungumza mara baada ya kukagua uwanja huo Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa amesema kuwa ukarabati huo utahusisha njia ya kuruka na kutua ndege, maeneo ya maegesho pamoja na barabara yenye urefu wa km 1.5 inayoingia katika uwanja huo.
Waziri huyo amesema kuwa “Tunategemea mwisho wa mwezi huu kutangaza zabuni ya ukarabati wa uwanja huu, matumaini yetu tutampata mkandarasi mzuri kwa ajili ya kazi hii,”.
Waziri Mbarawa alifafanua kuwa Serikali itahakikisha kuwa inajenga uzio katika uwanja huo ili kuhakikisha usalama wa uhakika uwanjani hapo.