Mwanamuziki wa Bongo Fleva anayekuja kwa kasi, Rummy amesema watu wamekuwa wakimuhusisha na biashara ya dawa za kulevya kutokana na muonekano wake.

Kauli ya mwanamuziki huyo inakuja kufuatia kuenea taarifa kuwa mwanamuziki huyo ni miongoni mwa wasanii wa Bongo Fleva wanaojihusisha na uuzaji na utumiaji wa dawa za kulevya.

Rummy ambaye anatamba na wimbo wake ‘Mwari’ aliomshirikisha Linah amesema kuwa kutokana na maisha yake na muonekano wake watu wamekuwa wakimuhusisha na biashara hiyo haramu kitu ambacho sio kweli.

Msanii huyo amesema kutokana na skendo hiyo kuwa kubwa alishawahi kuitwa na vyombo vya usalama na kuhojiwa juu ya sakata la uuzaji wa dawa za kulevya lakini anashukuru suala hilo lilikwisha salama na vyombo vya usalama viliona hausiki na mambo hayo.

Rummy amekiri wazi kuwa tetesi hizo zimekuwa zikumuharibia kwani kuna wakati anashindwa kuwa huru na kufanya mambo yake kwa uhuru kutokana na maneno ya watu, ila anadai katika maisha yake yeye anapenda sana kusafiri, kula vizuri, kuwa sehemu nzuri

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *