Rais wa Venezuela, Nicolas Maduro ameitaka marekani kuomba msamaha na kuondoa vikwazo dhidi ya makamu wake wa rais, Tareck El Aissami.
Markani inamshutumu Tareck El Aissami kwa kuhusika na ulanguzi wa dawa za kulevya nchini humo.
Maduro amesema anamuunga mkono kwa dhati Bw El Aissami ambaye ametaja hatua ya Washington kama uchokozi wa kibeberu.
Wizara ya fedha Marekani ilisema Tareck el-Aissami ni mlanguzi mkuu wa dawa za kulevya na amekuwa akifanya kazi na walanguzi Mexico na Colombia kusafirisha mihadarati hadi Marekani.
Vikwazo alivyowekewa vinahusisha kuzuiwa kwa mali yake Marekani na pia amepigwa marufuku kuzuru taifa hilo.
Marekani imesema amekuwa akilipwa na mlanguzi mkuu wa dawa za kulevya nchini Venezuela, Walid Makled ili kulinda mihadarati yake inapokuwa inasafirishwa.