Kamishna wa Mamlaka ya kuthibiti Dawa za Kulevya nchini, Rogers Sianga amesema kuwa majina ya mahakimu na majaji ambao wamevuga kesi za watu wanaotuhumiwa kujihusisha na dawa za kulevya kukabidhiwa Jaji Mkuu.
amesema hayo jana wakati wa mkuatano wa viongozi mbalimbali wa kitaifa na waandishi wa habari ulioandaliwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kwa ajili kupambana na dawa za kulevya.
Sianga amesema kuwa kesi zimevurugwa na mahakimu na majaji. hivyo wale wote wanaohusika watashitakiwa na hata wawe na mali ambazo wamezipata kwa biashara hiyo zitataifishwa.
Amesema kuwa watazunguka katika maeneo mbali mbali ya jiji la Dar es Salaam ili kuhakikisha mtandao huo unapatikana na kwenda hata Zanzibar na mbinu zote wanazijua katika kufanya biashara hiyo.