Bondia wa Ufilipino Manny Pacquiao amewata mashabiki wake wa kwenye mtandao wa kijamii wa Twitter kumchagulia bondia wa kupambana naye katika mchezo ujao wa kutetea ubingwa wake WBO.
Pacquiao amewataja mabondia hao ambao ni Amir Khan na Kell Brook, wa Uingereza, Jeff Horn wa Australia na Terence Crawford, wa Marekani.
Pacquiao amesema pambano hilo la kutetea mkanda ambao alishinda katika mwezi wa Novemba mwaka uliopita, litafanyika katika nchi za falme za kiarabu.
Bondia huyo mwenye umri wa miaka 38, na bingwa mara 6 wa dunia, alitangaza kustaafu katika mwezi wa Aprili, mwaka uliopita, lakini alirejea tena ulingoni na kumshinda Jessie Vargas mwezi wa Novemba, mwaka jana.