Walimu wilayani Korogwe mkoani Tanga wameshindwa kuishi kwenye shule walizopangiwa kutokana na uhaba wa nyumba za Walimu Wilayani humo.
Hayo yalisemwa na Kaimu Ofisa Elimu Sekondari wa Halmashauri ya Korogwe, Martha Kusare, wakati wa upokeaji majengo matatu ya maabara yaliyojengwa na Taasisi isiyokuwa ya kiserikali ya Vuga Development Initiative ya mkoani Arusha, ikishirikiana na A Better World kutoka nchini Canada kwa Shule ya Sekondari ya Patema iliyopo Kata ya Mpale.
Amesema hali hiyo imekuwa kikwazo kikubwa cha wanafunzi kushindwa kufikia malengo yao ya kitaaluma na kuiomba Serikali kuona namna bora ya kuanzisha ujenzi wa nyumba za walimu kwenye maeneo ya vijijini, kwani kuna uhaba mkubwa kutokana na kukosekana hata nyumba za kupangisha.
Pia amesema kitendo cha kukosekana kwa nyumba za walimu kwenye maeneo ya shuleni kumechangia hata kuwapo kwa tatizo la utoro wa wanafunzi wao na hivyo kama halmashauri wamejipanga kukabiliana nalo kwa vitendo ili kulimaliza