Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta ametoa onyo kali kwa watendaji wa serikali wasio waaminifu ambao wana dhamira ya kujinufaisha kwa namna yoyote na hali ya ukase iliyolikumba taifa hilo.

Rais Kenyatta ametoa onyo hilo wakati akitangaza janga la kitaifa la njaa kufuatia ukame mkubwa kuathiri nusu ya kaunti za nchi hiyo.

Sitomvumulia yeyote ambaye atajaribu kuchukulia hali hii kama fursa ya kujinufaisha na kuiba pesa za umma

Nazitaka taasisi zote za uchunguzi ikiwemo Tume ya Maadili na Kupambana na Rushwa zihusike kwenye shughuli zote zinazofanyika wakati huu. Sitaki kuona Serikali inatuhumiwa kutumia hali hii kwa manufaa yake’

Onyo hilo limekuja kufuatia mashirika ya kimataifa ya ‘International Federation of Red Cross’ na ‘Red Crescent Societies’ takiripoti kuwa zaidi ya watu milioni 11 nchini Kenya, Ethiopia na Somalia wanakabiliwa na njaa kali na wanahitaji msaada wa haraka wa huduma za kibinadamu kutokana na hali ya ukame.

Inadaiwa kuwa hali ni mbaya zaidi nchini Somalia ambapo takribani 40% ya raia wa nchi hiyo wanahitaji aina yoyote ya msaada wa kibinadamu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *