Jeshi la Polisi mkoani Kilimanjaro limetaja majina ya watu 47 wanaotuhumiwa kuhusika na usafishaji, kuuza na utumiaji wa dawa za kulevya huku wakikamata misokoto ya baingi zaidi ya 269.
Kukamatwa kwa watuhumiwa hao kumetokana na msako mkali uliofanywa na kikosi maalumu cha jeshi la Polisi mkoani humo kwa muda wa siku nne.
Kamanda wa Polisi mkoani Kilimanjaro, Kamishna mwanamizi wa Polisi, Wilbroad Mutafungwa amesema kuwa watuhumiwa hao tayari wamekamatwa na wapo katika hatua mbali mbali za kiupelelezi ili sheria ifuata mkondo wake kwa kufikishwa mahakamani.
Katika watuhumiwa hao wapo watoto wenye umri wa miaka 17 ambao wamekamatwa katika halmashauri ya Moshi.
Pia katika watuhumiwa hao wanawake wapo 15 ambao na wanaume 32 ambao wamekamatwa katika msako huo akiwemo mzee mwenye umri wa miaka 60.