Mwanamuziki mkongwe wa Bongo Fleva, Rehema Chalamila maarufu kama Ray C amesema kuwa kwa sasa hayuko kwenye mahusiano ya kimapenzi na mwanaume yeyote.
Ray C amesema kuwa sababu za kuamua kuishi bila mpenzi ni kwasababu anataka kwanza arudi katika hali yake kama zamani baada ya kutoka kwenye janga la utumiaji wa dawa za kulevya.
Msanii huyo aliyewahi kutikisa na ngoma kadhaa za bongo fleva zenye ujumbe wa mahaba kama vile Wanifuatia nini, Na wewe milele n.k atatikisa jukwaa la Azura Jumanne katika usiku wa Valentine, ambapo amesema amepania kutoa burudani kali kutokana na kukaa muda mrefu bila kufanya show,
Ray C amesema ana hamu ya kurudi kwenye game na tayari amesharekodi nyimbo kadhaa, lakini alishauriwa aanze na Valentine kwanza.
Ray C alitakiwa kutoa maoni yake kuhusu Msanii Recho ambaye amekuwa akifuata nyayo zake kuhusu kutajwa kwake kwenye orodha ya watu wanaohusika na dawa za kulevya, lakini alisema hawezi kuzungumzia suala hilo kwa kuwa hana uhakika juu ya suala hilo