Raia wameandamana nchini Mexico kupinga sera za uhamiaji za rais wa Marekani, Donald Trump pamoja na mpango wake wa kujenga ukuta katika mpaka wa mataifa hayo mawili.

Waandamanaji hao wameandamana katika miji kumi ya Mexico wakiwa wamevalia mavazi meupe na kupeperusha bendera za Mexico na kubeba mabango ya kumshutumu Trump.

Pia walimshutumu Rais Enrique Pena Nieto kwa kutokabiliana vilivyo na rushwa na ongezeko la uhalifu wa kutumia mabavu.

Waandamanji katika mji mkuu wa Mexico City wamebeba mabango ya kuonyesha umoja wao wa kupinga sheria hizo za Trump.

Trump anapanga kujenga ukuta mpaka wa Marekani na Mexico na amekuwa akisisitiza kwamba raia wa Mexico ndio watalipia ujenzi huo.

Hilo limewakera taia wa Mexico na rais Pena Nieto mara kwa mara amesisitiza kwamba taifa lake halitalipia ukuta huo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *