Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt . John Magufuli ameweka wazi sababu ya kuteua mwanamke katika nafasi ya Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, kuwa ni kutokana na kwamba wanawake wengi ni waaminifu katika suala la fedha.

Rais Magufuli amesema hayo Ikulu Jijini Dar es Salaam, muda mfupi baada ya kumuapisha Dkt. Anna Peter Makakala kushika nafasi hiyo.

Mara baada ya kumuapisha, Rais Magufuli amemtaka Kamishna huyo kufanya mabadiliko makubwa ndani ya Idara ya Uhamiaji nchini kutokana na utendaji wake kutoridhisha.

Hafla ya kuapishwa kwa viongozi hao pamoja na kula kiapo cha uadilifu kwa viongozi wa umma kilichoongozwa na Kamishna wa Maadili Mhe. Jaji Mstaafu Harold Nsekela, imehudhuriwa na Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa, Kaimu Jaji Mkuu Mhe. Prof. Ibrahim Juma, Mawaziri, Makatibu Wakuu wa Wizara mbalimbali na Wakuu wa vyombo vya Ulinzi na Usalama.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *