Zaidi ya watu 130,000 katika jimbo la California nchini Marekani wametakiwa kuhama makazi yao baada ya bwawa refu zaidi Marekani, Oroville kukabiliwa na hatari ya kubomoka.

Wahandisi waligundua kwamba vipande vikubwa vya saruji vilikuwa vimebambuka kutoka kwenye mtaro wa kuondosha maji kwenye bwawa hilo.

Watu wanaoishi katika maeneo ambayo huenda hakakumbwa na amfuriko bwawa hilo likiporomoka wametakiwa kuhama mara moja.

Viwango vya maji katika bwawa hilo vimepanda sana kutokana na mvua kubwa pamoja na theluji, baada ya miaka mingi ya kiangazi Valifornia.

Mara ya kwanza kwa Ziwa Oroville kukumbwa na dharura ya aina hiyo katika miaka 50 tangu kujengwa kwa bwawa hilo.

Idara ya maji na maliasili katika jimbo la California ilisema kwamba inaachilia karibu futi 100,000 mche mraba (mita 2,830 mche mraba) kila sekunde kupitia mtaro mkuu wa kuondosha maji kwenye bwawa hilo kujaribu kupunguza kiwango cha maji kwenye bwawa hilo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *