Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba amevunja ukimya baada ya kuongelea sakata la dawa za kulevya linaloendelea nchini.
Mwigulu ameongelea suala hulo la madawa ya kulevya wakati alipotakiwa kuongelea masuala ya wizara yake ndani ya Bunge siku ya jana.
Waziri huyo ameamua kuvunja ukimya huo baada ya kukutana na maswali kwanini hajaonekana akiongelea sakata la dawa za kulevya toka limeibuka Dar es Salaam wakati yeye ni waziri wa Mambo ya Ndani.
Mwigulu amesema kuwa lililoongelewa sana ni hili la dawa za kulevya, vita ya dawa za kulevya ni vita ya kila Mtanzania na haijaanza sasa, mimi tangia nilipofika nilikuta tayari Mh. Kitwanga ameshakamata Mapapa Wakubwa tu na tulivyotoka pale tumeendeleza.
Pia ameongeza kwa kusema ninachowaambia Waheshimiwa Wabunge tunaweza kutofautiana mtazamo kwenye approach na nyinyi kama Wabunge na Washauri wetu mkitushauri njia nzuri za kufanikisha jambo hili sisi mara zote tutakua tunapokea ushauri huo sababu vita hii ni yetu sote.
Aliongeza kwa kusema kuwa Jambo moja tu ambalo nawahakikishia na ambalo nawaomba wote tuwe nalo, tusibadili lengo… na kuna watu wengine walikua wanasema mbona Waziri hujasema? ……..nimeshazunguka mikoa yote kasoro Njombe, Ruvuma, Singida na Songwe, kwenye mikoa yote huko nimetoa maelekezo ya kufanyiwa kazi, mojawapo ni dawa za kulevya.
Mwisho alimaza kwa kusema kuwa nikishatoa maelezo kama hayo sibinafsishi tena hiyo shughuli, Mtanzania ambaye inamuhusu popote alipo lazima tusimamie mambo haya kwa upana wake, Waheshimiwa Wabunge katika maswala haya ya kitaifa tushirikiane wote, watu huwa hawagombani kwa ajili ya kazi watu huwa wanasaidiana kazi.