Jeshi la Polisi mkoani Mwanza linamshikilia mtu mmoja, Hemed Kesi mwenye umri wa miaka 43 mkazi wa Kanyerere kwa kosa la kupatikana na dawa za kulevya aina ya heroine kiasi cha pinchi 240.

Taarifa iliyotolea na jeshi la mkoani humo limesema kuwa mtu huyo ni  mfanyabiashara wa spear za magari katika mtaa huo wa Kanyerere mkoani Mwanza.

Kwa upande wake Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza DCP Ahmed Msangi amesema kuwa awali polisi walipata taarifa za mtuhumiwa huyo kuwa anajihusisha na biashara ya madawa ya kulevya, hivyo askari walikuwa wakiendelea na upelelezi pamoja na uchunguzi kuhusiana na  tuhuma hizo.

Kamanda huyo amesema kuwa wakati askari wakiendelea na upelelezi dhidi ya tuhuma za mfanyabiashara huyo polisi walipokea taarifa kutoka kwa raia wema kwamba mtuhumiwa huyo ameingiza mzigo mkubwa wa madawa ya kulevya kutoka Dar es Salaam na ameanza kuusambaza mtaani.

 

 

 

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *