Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta ametangaza hali ya ukame kuwa janga la kitaifa nchini humo kutokana na hali ya jangwa.

Hali hiyo inafuatia ukame uliokithiri nchini humo kwa zaidi ya nusu mwaka, huku majimbo 23 kati ya 47 ya nchi hiyo kukumbwa na baa la njaa.

Kumeshuhudiwa uhaba mkubwa wa chakula hasa katika maeneo ya kaskazini mwa taifa hilo ambayo yameshuhudia ukosefu wa mvua huku wanyama na raia wakifa.

Naomba sote tuyachunguze mashirika likiwemo tume ya kupambana na ufisadi (EACC) kuwa katika mstari wa mbele kukabiliana na wafisadi wakati wote wa usambazaji chakula cha msaada. Sitaki serikali ilaumiwa kwa kuchukua nafasi hii eti inawapunja raia.” Uhuru Kenyatta alisema.

Onyo hilo linatukia wakati ambapo shirika la kimataifa la msalaba mwekundi na lile la Red Crescent, zikionya kuwa Zaidi ya watu milioni 11 kutoka Kenya, Ethiopia na Somalia wamo katika hatari ya kufa njaa na wanahitaji kwa haraka msaada wa kibinadamu, kutokana na kukithiri kwa ukame.

Nchini Ethiopia, ukame mmbaya kwa zaidi ya karne moja ulikithiri nchini humo, kwa pamoja na mmiminiko wa watu waliokimbia vita nchini Somalia, shirika la msalaba mwekundu umeonya.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *