Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa amesema atamuagiza Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG)  kuchunguza ukusanyaji wa mapato ya Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL).

Waziri mkuu ametoa kauli hiyo jana alipotembelea Makao Makuu ya shirika hilo Jijini Dar es Salaam kwa lengo la kujionea mwenendo wa uendeshaji wake.

Pia amesema serikali haiko tayari kuona shirika hilo linakufa tena, hivyo amewataka viongozi wake wahakikishe linaendeshwa kwa mafanikio kwa manufaa ya Taifa.

Majaliwa amewataka wafanyakazi wa Shirika hilo waache kukusanya mapato kwa kutumia risiti za kuandika kwa mkono na badala yake waanze kutumia mfumo wa kieletroniki ili kuzuia upotevu wa mapato hayo.

Waziri Mkuu amemtaka Kaimu Mkurugenzi wa Fedha na Utawala wa ATCL, Witness Mbaga ajiridhishe na fedha zinazokusanywa katika eneo la mizigo kama ziko sahihi ili kudhibiti upotevu wa mapato.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *