Wabunge wa Bunge la Afrika kusini wamefanya vurugu Bungeni kuipinga hotuba ya Rais wa nchi hiyo Jacob Zuma alipokuwa anahutubia Bunge hilo hapo jana.
Rais Zuma alipata wakati mgumu baada ya kuanza kuhutubia alikatizwa na kelele za Wabunge wa upinzani waliokuwa wakimkosoa wakati wa hotuba hiyo hali iliyisababisha kutokuwa na maelewano Bungeni humo.
Wabunge hao wa upinzani walikosoa kuhusiana na matatizo ya kiuchumi na rushwa, ulifanywa pia na baadhi ya wabunge kutoka chama tawala ambapo wanaonekana kutokubali uongozi wa Zuma.
Nje ya bunge la nchi hiyo, Polisi walifyatua mabomu kuwashtua watu waliokuwa wakifanya vurugu ili kuweza kuwasambaratisha na kurudisha hali ya kawaida Bungeni hapo.
Kabla ya kuanza kwa hotupa hiyo Rais Jacob Zuma alipeleka kikosi cha wanajeshi zaidi ya elfu nne bungeni hapo ili kulinda usalama, wakati akitoa hutuba yake.