Staa wa filamu za Johnny Depp ameanza kuuza nyumba zake za kifahari baada ya hali ya kifedha kuzidi kuwa mbaya.

Staa huyo ambaye ana kesi mahakamani dhidi ya kampuni ya The Management Group aliyoishtaki kwa kumsababishia hasara na kudai fidia ya $25m ameuza jumba lake lililopo Los Angeles kwa thamani ya $2.5.

Depp anadaiwa kununua jumba hilo kwa $7.2m kati ya mwaka 2007 na 2008.

Jumba hilo linalodaiwa kuwa na mgawanyo wa nyumba tano ndani yake ndilo jumba kubwa zaidi la staa huyo na anadaiwa kuuza nyumba kubwa zaidi kati ya tano zinazounganisha jumba hilo.

Inadaiwa kuwa staa huyo alitaka bei ya jumla kwa nyumba zote tano iwe $12.78m lakini hakubahatika kupata mteja wa aina hiyo hivyo akaamua kuuza sehemu moja ya nyumba hiyo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *