Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu amepewa dhamana na Mahakama ya Hakimu Mkazi baada ya kukizi vigezo vya dhamana na kutoa milioni 20.

Tundu Lissu alipandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akikabiliwa na mashtaka manne ya uchochezi.

Wakili wa Serikali Kishenyi Mutalemwa  aliwasilisha maombi ya kupinga dhamana yaTundu Lissu kwa madai kwamba   amekuwa na mwenendo unaohatarisha amani si tu kwa wanajamii, bali hata kwake mwenyewe kwa kuendelea kutoa maneno ya uchochezi.

Hakimu Huruma Shaidi, ametupilia mbali ombi hilo la serikali na kumpa  Tundu Lissu dhamana ya sh. Milioni 20.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *