Rais wa Gambia, Adama Barrow amesema kuwa nchi hiyo haitajiondoa kutoka mahakama ya kimataifa ya makosa ya jinai, (ICC).
Barrow alishinda uchaguzi mkuu wa Disemba 1, 2016, kwa ahadi ya kupigania haki za binadamu na uhuru, na kumaliza unyanyasaji ambao raia wa Gambia wamepitia wakati wa utawala wa miaka 22 wa Bw Jammeh.
Naye mwaandishi mmoja wa habari wa Uingereza nchini Gambia, ameandika katika mtandao wake wa Twitter kuwa Jumuia ya bara Ulaya, imeahidi kuzidisha mara dufu msaada wake kwa taifa hilo dogo la Afrika Magharibi.