Staa wa Pop, Madonna amethibitisha kuasili watoto wawili mapacha nchini Malawi kupitia akaunti yake ya Instagram.

‘Nimefurahi sana na ninashukuru kwa kila mmoja miongoni mwa wamalawi aliyepelekea kufanikiwa kwa jambo hili’. Ameandika Madonna.

Pamoja na ujumbe huo, Madonna pia ameviomba vyombo vya habari vimpe uhuru binafsi katika kipindi hiki cha mpito.
Madonna alipata ridhaa ya mahakama ya kuasili watoto hao siku ya Jumanne wiki hii.

Tayari Madonna ana watoto wawili wa kuasili kutoka nchini Malawi, David na Mercy ambao alikabidhiwa mwaka 2006 na mwaka 2009.

Mwishoni mwa wiki iliyopita Madonna alikanusha kuwasilisha ombi la kuasili watoto hao baada ya taarifa ya msemaji wa Serikali kudai staa huyo amewasilisha maombi ya kuasili watoto wengine.

Hata hivyo nyaraka za mahakama zimeonyesha kuwa Madonna alijisikia kuhitajika kuasili watoto hao kutoka kituo cha watoto yatima baada ya kupata taarifa za kina kutoka kwenye taasisi yake ya kusaidia watoto nchini humo.

Watoto aliowaasili sasa ni mapacha Esther na Stella ambao mama yao alifariki kifo cha uzazi baada ya kujifungua watoto hao.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *