Rais wa Afrika Kusini, Jacob Zuma ameviagiza vikosi vya kijeshi vipatavyo 440 kulinda usalama katika majengo ya bunge wakati wa hotuba yake leo.

Hotuba za hapo awali za Zuma, zilikumbwa na maandamano na fujo, huku wabunge wa upinzani wakitoa wito wa kujiuzulu kwake.

Taarifa kutoka kwa Ofisi ya rais na iliyotolewa siku ya Jumanne, inasema kuwa Bw Zuma aliamrisha kutumwa kwa vikosi hivyo vya wanajeshi, ili kushirikiana na maafisa wa polisi kutoa ulinzi.

Hii ni mara ya kwanza kwa wanajeshi wa nchi hiyo, kudumisha usalama, badala ya kuhusika katika sherehe.

Kwa mujibu wa taarifa zilizochapishwa katika vyombo vya habari nchini humo, duru za kiusalama zimeonya kuwa kutatokea maandamano makubwa katika hafla hiyo.

Duru hizo zilisababisha hofu, kwamba huenda polisi wakashindwa kukabiliana nayo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *