Mwanasiasa na kiongozi mkuu wa upinzani nchini Urusi, Alexei Navalny, amekutwa na hatia ya matumizi mabaya ya fedha na kuhukumiwa kutoshiriki siasa kwa miaka mitano.

 Hukumu hiyo inamfanya mwanasaisa huyo kukosa vigezo vya kushindana na rais Vladimir Putin kwenye uchaguzi wa mwakani.

Navalny alikutwa na hukumu hiyo ambayo ilitolewa kwenye marudiao ya kusikilizwa kwa kesi yake ambapo hukumu ya awali ilipingwa na Mahakama ya Ulaya ya Haki za Binadamu na kudaiwa haikuwa hukumu ya haki.

Hata hivyo mwanasiasa huyo ameendelea kumshutumu rais Putin na kudai madai aliyohukumiwa nayo ni ya uongo na kesi yake ina mkono wa kisiasa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *