Staa wa filamu za Battlestar Galactica, Richard Hatch amefariki dunia kwa ugonjwa wa kansa ya kongosho akiwa na miaka 71.

Staa huyo ambaye ndiye staa pekee aliyeshiriki kwenye filamu mbili za Battlestar Galactica, halisi na mpya ilitolewa siku za karibuni alikuwa akiigiza kama Kapteni Apollo kwenye toleo la kwanza la mfululizo wa filamu hiyo ya aina ya sci-fi kisha akaigiza kama Tom Zarek kwenye toleo la pili la filamu hiyo iliyotoka mwaka 2009.

Tayari mastaa wengine wa filamu wameanza kutuma salamu za rambirambi huku staa wa Star Trek, George Takei akiandika kwenye Twitter: ‘Rest with the galactic stars, Richard Hatch.’

Staa mwingine aliyetuma salamu hizo ni Ronald D Moore, ambaye aliitengeneza toleo la pili la Galactica, akimuelezea Hatch aliandika: ‘a good man, a gracious man, and a consummate professional. His passing is a heavy blow to the entire BSG family’.

Mtoto wa staa Hatch, Paul ndiye aliyethibitisha kutokea kwa kifo cha baba yake kwa kuandika kwenye tovuti ya staa huyo:

‘He died peacefully with his family and friends at his side after a battle with pancreatic cancer.’

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *