Kamanda wa polisi eneo la Laikipia nchini Kenya, Mbelengo Mohare amepigwa risasi wakati wa mapigano na wafugaji nchini humo.
Mbelengo Mohare, alikuwa akiongoza oparesheni dhidi ya wafugaji ambao walikuwa wamevamia mashamba ya kibinafsi miezi ya hivi karibuni.
Alipelekwa kupata matibabu hospitali iliyokuwa karibu kalba ya kusafirishwa hadi jijini Nairobi kwa matibabu zaidi.
Kamishina wa eneo hilo Onesmus Musyoki, anasema kuwa oparesheni hiyo bado inaendelea kutokana na wafugaji hao kugoma kuondoka eneo hilo.