Mahakama ya Rufaa nchini Marekani imewajia juu wale wanaopinga na wanaotetea katazo la liliyotolewa na Rais Donald Trump kwa raia wa mataifa saba yenye Waislamu wengi kutoingia mahakamani.

Katazo hilo limewataka wahamiaji na wageni kutoka nchi hizo saba – Iran, Iraq, Libya, Somalia, Sudan, Syria na Yemen – kuingia Marekani, lakini utekelezaji wake ulisitishwa na mahakama wiki iliyopita.

Jopo la majaji watatu limeuliza maswali kuhusu upeo na kikomo cha madaraka ya rais na ushahidi ambao Bw Trump alitumia kufanya uamuzi huo.

Aidha, majaji hao wameuliza maswali kuhusu iwapo hatua hiyo inafaa kuchukuliwa kuwa ubaguzi.

Bila kujali uamuzi wa mahakama hiyo, iwapo itaunga mkono au kupinga amri hiyo ya Bw Trump, kuna kila dalili kwamba kesi hiyo itapelekwa Mahakama ya Juu.

Kulikuwa na kipindi cha kila upande kueleza na kufafanua msimamo wao Jumanne.

Wizara ya haki (serikali) ilikuwa ya kwanza kujitetea, ambapo mawakili wake waliwahimiza majaji kurejesha marufuku hiyo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *