Muigizaji nyota wa Bongo movie, Irene Uwoya amesema kuwa katika mahusiano ya kimapenzi anavutiwa sana na wanaume wasiokuwa na sura za mvuto.

Uwoya amefunguka hayo na kuweka wazi sababu inayomfanya kuwapenda sana wanaume wenye sura mbaya au wanaume ambao hawana muonekano mzuri kwa sura na kusema ndiyo watu ambao huwa wanamchanganya.

Pia amesema kuwa wanaume wenye sura mbaya ni kati ya watu ambao huwa wanamuhamasisha sana kwenye mapenzi na kudai yeye havutiwi kabisa na watu wenye sura nzuri.

Muigizaji huyo ameongeza kwa kusema kuwa “Kitu ambacho hamkijui kuhusu mimi ni kuwa sijawahi kuvutiwa na wanaume wenye muonekano mzuri, sielewi ni kwanini lakini wanaume wenye sura mbaya huwa wanaamsha hisia zangu za kimapenzi”.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *